Opening Hours

8:00 am to 5:00 pm

info@thesuperteam.co.tz

(+255) 716 160 141

Uhindini Street

Dodoma, Tanzania

UTAWEZAJE KUNUFAIKA NA SEKTA YA KUPUNGUZA UZITO?

 

UTAWEZAJE KUNUFAIKA NA SEKTA YA KUPUNGUZA UZITO?

 

Katika karne hii ambapo changamoto ya watu kua na uzito mkubwa imezidi changamoto ya watu wanaopata madhara kutokana na kuvuta sigara, ni wakati sahihi mno kwa mtu yoyote mwenye jicho la tatu la kukamatia fursa. Inawezekana wewe mwenyewe ni mtu unaehitaji kupungua uzito au huhitaji kupungua uzito, bado kuna nafasi sawa kabisa ya kuwa sehemu ya sekta hii inayokua kwa kasi sana. Ninachotaka kukwambia tu ni kwamba unaweza kupungua uzito na huku ukijiongezea kipato kupitia kupungua kwako.

 

Sasa hivi, ukipita mitandaoni utaona watu wengi sana wakitangaza namna unaweza kupunguza uzito wako, ambapo utatakiwa kununua program zao za kupunguza uzito, kimsingi zipo ambazo zitakupa matokeo mazuri na zipo ambazo hazitakupa matokeo mazuri. Lakini kama itatokea utapata matokeo mazuri kwa kupungua uzito unaoutaka, bila shaka utafurahia mwili wako mpya ulioupata baada ya kupungua. Lakini pia ni vyema ukatambua kua huyo alie kuuzia hiyo program ataendelea kupata pesa nyingi zaidi kupitia matokeo yako mazuri ya kupungua uzito wako.

 

 •          KUWA MSHAURI WA WATU WANAOTAKA KUPUNGUA UZITO

 

Kama nilivyosema awali, sekta hii inakua kwa kasi sana, maana yake kuna watu wengi sana ambao wanahitaji msaada wa kupunguza uzito na ulaji mzuri; tafiti zinasema kwamba kati ya watu 10, kuna watu 6 wenye uzito mkubwa, na hawa ni watu ambao wanatumia pesa nyingi sana kuhakikisha wanarudisha miili yao iliyo na uzito unaotakiwa, ingawa wengi wao hawafanikiwi kwakua wanakosa program sahihi za kuwasaidia kupungua na kudhibiti uzito baada ya kupungua, lakini pia wanakosa watu wenye uelewa na elimu sahihi kuhusiana na kupunguza uzito na ulaji ulio mzuri.

 

Sasa hii ni nafasi kwako, kwasababu utapana nafasi ya kuwa na program ambayo duniani kote inasifika kwa ubora wake lakini pia hasa kwa kuboresha afya ya mtumiaji wa program kwa kipindi chote atakachokua anafanya program, lakini pia kumpatia matokeo halisi ya kupungua uzito. Kikubwa zaidi, hautapata program peke yake, lakini pia kupitia uzoefu uliopitia wakati unaifanya program yako ya kupunguza uzito ambapo utakua ukipewa mwongozo, msaada na elimu sahihi juu ya kupunguza na kudhibiti uzito; hiyo itakusaidia kuweza kupata mwanga na kuweza kuwasaidia wengine. Lakini pia utakapo amua kuwa mshauri wa watu wanaotaka kupunguza uzito, utaendelea kupata mafunzo na mwongozo kuhusiana na masuala yote ya kupunguza na kudhibiti uzito.

 

Pamoja na hayo utaoneshwa njia mbalimbali za kukuwezesha kuwafikia wahitaji wa kupungua uzito, ikiwa ni pamoja na mwongozo wa nini ufanye kila siku ili uweze kuwafikiwa wahitaji wengi zaidi. Ni kwa muda mrefu sana nimekua nikisoma na kufatilia tafiti mbalimbali ambazo ni za muhimu ili kupata kukuwezesha kujenga biashara kubwa ya watumiaji wa program za kupunguza uzito. Huu mwongozo naweza kukiri ni wa kipekee na utaenda kufanya mapinduzi makubwa mno katika kuwasaidia wote wanaotaka kutengeneza kipato kwa kupitia program ya kupunguza uzito.

 

 •           NININI KILICHOPO KATIKA MUONGOZO WA KUWASAIDIA WANAOTAKA KUPUNGUA NA KUONGEZA KIPATO?

 

 • Makundi ya damu (Blood Groups) na vyakula vyao
 • Mpangilio wa mlo kwa makundi tofauti tofauti ya watu na malengo yao ya kupungua
 • Mazoezi muhimu ya kupunguza na kudhibiti uzito
 • Namna ya kuwafikia wahitaji wa kupungua uzito na wanaotaka kutengeneza kipato
 • Namna ya kuongeza kupato kupitia program ya kupunguza uzito
 • Mbinu muhimu za kutanua biashara yako

 

 

 •             NI KIASI GANI CHA PESA MTU ANAWEZA KUTENGENEZA ENDAPO ATAAMUA KUWA SEHEMU YA WATU WANAO SHAURI WENGINE KUPUNGUA UZITO?

 

Kimsingi, hakuna kipimo cha kiasi cha pesa ambacho mtu anaweza kutengeneza hapa, ila ni uwezo wako wa kuweza kuwasaidia watu wengine wengi wakatimiza malengo yao. Kwa idadi kubwa ya watu wanaohitaji kupungua na wanaohitaji kuongeza kipato chao, ni dhahiri una uwezo mkubwa sana wa kupata pesa nyingi endapo utafuatilia kwa makini yaliyomo kwenye mwongozo, na yale utakayopata kutoka kwangu ana kwa ana.

 

Mfano halisi; kama ukaamua kua sehemu ya hii biashara kwa asilimia 100% (kwa kuanza biashara hii kwa mtaji kamili ambao ni kwa kununua program ya kudhibiti uzito pamoja na bidhaa zingine za kuimarisha afya), utapata faida ya Tsh. 100,000 kwa kila program moja utakayoiuza kwa mtu ambae atahitaji program ili apungue tu basi; au utaweza kupata bonus ya Tsh. 90,000 kwa kila mmoja atakae amua kuwa sehemu ya biashara hii kwa kuamua kuchukua program ili apungue yeye mwenyewe ili baadae aweze kuwasaidia na wengine. Lakini kwa kuwasaida hawa walioamua kua sehemu ya biashara hii kwa kuhakikisha wanapata mwongozo na elimu sahihi katika kuwafikia wahitaji wengine wengi ziadi, utakua umejenga chanzo endelevu cha kipato kutokana na asilimia kadhaa utakazo kua unalipwa kutokana na manunuzi wanayo yafanya wao.

 

Kimsingi, unahitaji elimu zaidi juu ya hili. Usisite kunitafuta kupitia mawasiliano haya

 

Simu: 0716160141

 

Yours Truly,

 

Lusajo.

 

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE MicrosoftInternetExplorer4 /* Style Definitions */ table.MsoNormalTable {mso-style-name:"Table Normal"; mso-tstyle-rowband-size:0; mso-tstyle-colband-size:0; mso-style-noshow:yes; mso-style-priority:99; mso-style-qformat:yes; mso-style-parent:""; mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt; mso-para-margin:0in; mso-para-margin-bottom:.0001pt; mso-pagination:widow-orphan; font-size:10.0pt; font-family:"Calibri","sans-serif"; mso-bidi-font-family:"Times New Roman";}

NAMNA GANI UTAFIKIA LENGO LAKO LA KUPUNGUZA UZITO; MCHANGANUO WA KINA AMBAO KILA MTU ANAWEZA KUUMUDU

 

NAMNA GANI UTAFIKIA LENGO LAKO LA KUPUNGUZA UZITO; MCHANGANUO WA KINA AMBAO KILA MTU ANAWEZA KUUMUDU

Unapotaka Kupunguza uzito wako na kuanza diet, ni muhimu sana ukajua Upo katika kundi lipi kati ya Haya.

1. Je, Unataka diet ili kurejesha afya yako ambayo umeipoteza? kwa lugha ingine, tayari una changamoto za kiafya ambazo zimetokana na uzito mkubwa kama vile Kisukari, Pressure, Moyo, Magonjwa ya viungio kama mgongo, magoti n.k.

2. Je, Unahitaji Diet kwasababu Una dalili ambazo si Nzuri, kama vile kupata ganzi kwenye miguu na mikono, tumbo kujaa gas, kupunguza ufanisi kwenye tendo la ndoa, mapigo ya moyo kuenda kasi, kuchoka haraka, kupenda kula vitu vyenye sukari kama Keki, soda n.k.

3.e, unataka diet ili kurejesha lifestyle Nzuri, kuanzia kwenye ulaji wako, ufanyaji Mazoezi, Kunywa maji ya kutosha na kulala usingizi wa kutosha? Kwamba ukitazama namna lifestyle yako ilivyo unaona utaingia kwenye changamoto za magonjwa yatokanayo na uzito mkubwa

Ukishajua upo kundi gani inakua rahisi kujua ni diet yako itafanyika vipi, au pengine kabla ya diet kuna baadhi ya changamoto za kiafya ambazo inatakiwa zikae sawa kwanza kabla ya diet kuanza.

Baada ya hapa hakikisha unapata majibu ya haya maswali

1. Una uzito kg ngapi?

2. Unapenda kupungua kg ngapi?

3. Umeshawahi kutumia diet yoyote ili kupunguza uzito?

Hii itanisaidia kutambua ni mazoezi gani ufanye na pia kujua diet Plan itakayokufaa.

MCHANGANUO WA DIET NA GHARAMA ZAKE

Hapa kuna OPTIONS kadhaa, utaangalia ipi itakufaa kwa kuzingatia budget yako na kiasi cha uzito unaotaka kupungua.

1. OPTION YA KWANZA:

Kama unataka kupungua kuanzia 15kg na zaidi, hapa utahitaji kwanza kuanza na diet Plan ya kusafisha mwili wako ili sumu na uchafu ambacho ni kichocheo kikubwa sana cha kuongeza uzito wako. Baada ya Hii diet ya kusafisha mwili wako utaifanya kwa siku 9, ambapo itakusaidia kuondoa sumu Lakini pia utapungua uzito kuanzia 3kg hadi 8kg (itategemea na jinsi utakavyokua na nidhamu ya kufuata maelekezo na kufanya mazoezi). Diet hii inauzwa 320,000 Tsh.

Baada ya diet plan ya kusafisha mwili wako, utafanya diet Plan ya pili ya kupunguza uzito wako. Hii utaifanya kwa siku 15. Hapo utaweza kupungua uzito kuanzia 5kg hadi 15kg (itategemea na nidhamu yako ya kufuata diet na kufanya mazoezi). Diet hii inauzwa 400,000 Tsh.

Kwahiyo Gharama Diet Plan ya Option ya kwanza kwa Jumla ni 720,000 Tsh. Kwasababu baada ya diet plan hizi mbili, utaendelea na ratiba na utaratibu wa kupunguza vyakula vya wanga, mafuta na kuongeza vyakula vya protein na vitamins katika mlo wako; huku ukizingatia mazoezi ya kujiweka fit na kunywa maji ya kutosha.

KAMA BUDGET YAKO HAITOSHI  (huna 720,000) NA UNATAKA KUPUNGUA ZAIDI YA Kg 15?

Hapa unaweza kuchukua ile diet Plan ya kusafisha mwili tu ambayo inauzwa (320,000 Tsh.) ili ikusaidie kuondoa kikwazo namba moja cha kukufanya upungue. Ukimaliza hii Diet basi utaendelea na mpangilio mzuri wa ulaji (kupunguza wanga na mafuta na kuongeza protein na vitamins kwenye mlo wako, na pia kufanya mazoezi.

Lakini kumbuka hii itakuchukua muda mrefu zaidi kufikia lengo lako la kupungua zaidi ya Kg15 tofauti na yule atakaechukua diets zote mbili.

2. OPTION YA PILI

Kama unataka kupungua kati ya 3kg hadi 10kg, hapa utahitaji kwanza kuanza na diet Plan ya kusafisha mwili wako ili sumu na uchafu ambacho ni kichocheo kikubwa sana cha kuongeza uzito wako. Baada ya Hii diet ya kusafisha mwili wako utaifanya kwa siku 9, ambapo itakusaidia kuondoa sumu Lakini pia utapungua uzito kuanzia 3kg hadi 8kg (itategemea na jinsi utakavyokua na nidhamu ya kufuata maelekezo na kufanya mazoezi). Diet hii inauzwa 320,000 Tsh.

Baada ya kuimaliza hii Diet basi utaendelea na mpangilio mzuri wa ulaji (kupunguza wanga na mafuta na kuongeza protein na vitamins kwenye mlo wako, na pia kufanya mazoezi.

KAMA BUDGET YAKO HAITOSHI (huna 320,000 Tsh.) NA UNATAKA KUPUNGUA 3kg hadi 10kg)?

Hapa unaweza chukua sehemu ya virutubisho ambavyo vipo Kwenye ile diet Plan ya kusafisha Mwili. Ambapo Utachukua (Aloe Vera Gel Juice mbili na Garcinia Plus Moja) ambazo zote 225,000 Tsh. Ambapo Juice utazitumia ndani ya week moja. Na Garcinia Plus utaitumia hadi mwezi mmoja. Kwahiyo option hii itakufanya uendelee na Diet hadi siku 30. Ambapo kimsingi mazoezi ndiyo yatakusaidia kukupa matokeo, lakini pia Garcinia itasaida kuyeyusha mafuta Kila ufanyapo Mazoezi na aloe Vera Gel itakusaidia kusafisha sumu na uchafu mwilini. Lakini katika hiki kipindi chote utatakiwa kupunguza wanga na mafuta  kwenye mlo wako na pia kutotumia kabisa wanga wakati wa chakula cha usiku. Tumia zaidi Protein na vitamins .

3. OPTION YA TATU

Kama Unataka kupungua kati ya kg 1 hadi 3kg. Hapa utahitaji kutumia Garcinia Plus na Mazoezi zaidi. Garcinia itakusaidia kuyeyusha mafuta mwilini hasa unapokua unafanya Mazoezi. Na itakusaidia kubalance kiwango cha appetite yako kukaa sawa na pia kupunguza hifadhi ya wanga kua kwenye mfumo mafuta mwilini. Hapa utahitaji 85,000  Tsh. Ili kupata Garcinia Plus.

Pia ni muhimu kuzingatia Mazoezi na ulaji sahihi (punguza au Ondoa wanga Kwenye mlo wako, kunywa maji ya kutosha na pata usingizi wa kutosha).

ZINGATIA

OPTIONS zote hizi tatu zimezingatia idadi ya uzito unaotaka kupungua na uhalisia na ukweli wake wa kufikia lengo la kupungua. Kwasababu nguzo kuu ya kufanya mtu apungue ni kwa kuondoa sumu mwilini. Kwasababu binadamu tunaingiza sumu nyingi sana mwilini, takribani lita mbili za simu tunaziingiza katika miili yetu Kila mwaka, kupitia vyakula, Vinywaji na hewa tunayovuta. Na hizi sumu sio tu zimekua ni chanzo cha magonjwa mengi bali pia inachangia mno kwenye kuongeza uzito kwa binadamu. Ndiyo sababu Kila option nimeangalia wingi wa kg ambazo Unataka kupungua na nimeweka Diet au virutubisho vitakavyokusaidia kusafisha hizo sumu.

Mwisho, ni kwamba unapokua unaanza Diet yako kumbuka lengo sio tu kupunguza uzito bali ni kubadili mfumo wako wa maisha kua unaojali afya yako zaidi; kwa kufanya mazoezi, kunywa maji ya kutosha, kupunguza wanga na mafuta katika mlo wako kwa kuongeza protein na kupata usingizi wa kutosha.

KWA MAELEZO ZAIDI: +255716160141 (Piga au WhatsApp)

Karibu sana.

MPANGILIO WA MLO HUU NA MAZOEZI HAYA YATAKUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO

 

MPANGILIO WA MLO HUU NA MAZOEZI HAYA YATAKUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO

Imekua ni changamoto duniani kote ambapo sehemu kubwa ya watu wanahangaika kurudisha uzito wao kwenye uwiano unaotakiwa. Ni jambo jema kuona jamii imeaka na kutambua umuhimu wa kutunza afya zao. Na ndiyo maana utaona kila kona kuna sehemu za kufanyia mazoezi (gym) na pia utaona watu mtaani wakifanya jogging asubuhi na jioni. Na pia utaona wengi wakitaka kujua ni namna gani wafanye ili kuweza kudhibiti ulaji wao na hatimaye kupunguza uzito au kubaki na uzito wao sahihi.

Kwa bahati mbaya watu wengi hukosa taarifa au maarifa sahihi ya kuweza kuwasaidia kupungua uzito, na hivyo kujikuta wakiingia kwenye matatizo ya kiafya kutokana na kujiingiza katika diet plans ambazo kwa sehemu kubwa zinazuia kula chakula na hivyo kuukosesha mwili viini lishe ambavyo kimsingi vinahitajika mwilini ili kuuwezesha mwili kufanya kazi zake kama kawaida.

Sasa kabla sijakujuza mpangilio wa mlo (diet plan) ambayo itakusaidia kupunguza uzito wako, kuna vitu inatakiwa uvijue kwanza. Ni vema ukajua kwanini unataka kuanza diet;  Je, ni unataka kuboresha afya yako (kwamba huna tatizo kwasasa, lakini ukijitazama mpangilio wako wa maisha ulivyo au kuna baadhi ya dalili mbaya umeanza kuziona na unaona kabisa siku za usoni utaingia kwenye matatizo ya kiafya kama hutachukua tahadhari sasa hivi. Au Pengine unataka diet ili uishi maisha ambayo ni salama zaidi kwa kuzingatia tahadhari zote ambazo zinaweza kukuingiza kwenye matatizo ya kiafya. Na mwisho kabisa ni unataka diet ili kurejesha afya yako ambayo umeipoteza, kwa lugha ingine, tayari una changamoto za kiafya ambazo zimetokana na uzito mkubwa kama vile Kisukari, Pressure, Moyo, Magonjwa ya viungio kama mgongo, magoti n.k.

Sasa basi, kama una uzito mkubwa na tayari una changamoto za kiafya kama vile Kisukari, Presha, Moyo, na magonjwa ya viungio kama mgongo na magoti na yapo katika hali mbaya zaidi, itakulazimu kwanza utibu matatizo hayo kabla hujaenda kuanza diet. Hii ni katika kukuza matatizo ambayo uliyonayo tayari kwasababu ya uzito. Lakini kama changamoto hizo ulizonazo zipo vizuri na hazikusumbui kwa maana ya kwamba umekua ukipata matibabu na hali ya magonjwa hayo imekaa vizuri, basi hapo utaweza moja kwa moja kuanza diet plan kwaajili ya kupunguza uzito.

MLO (DIET)

Kwanza inatakiwa uelewe kwamba diet zozote za kudhibiti uzito zina changamoto zake. Ni changamoto sana kwasababu sehemu kubwa ya vyakula vyake hua ni asilia na havitakiwi kupikwa, kuchomwa au kuchemshwa kwenye  joto zaidi ya sentigredi 48, pia havitakiwi kuwa ni vyakula ambavyo vimehifadhiwa kwa kutumia visindika, au katika uandaaji mashambani visiwe vilitumia mbolea na madawa ya kupuliza. Hii yote ni kuhakikisha kile unachoenda kukitumia kina kiasi cha kutosha cha viini lishe na pia hakina kemikali mbaya ambazo zitaenda kupunguza spidi ya kupungua uzito wako. Sasa hii changamoto sio ndogo, kwasababu sehemu kubwa ya vyakula tunavyovipata masokoni hata mashambani, vimetumia mbolea sana au madawa ya kupuliza, na hata vikifika majumbani, bado namna ya kuvipika imekua ni changamoto, wengi hujikuta wakitumia joto jingi ambapo sehemu kubwa ya viini lishe na madini na vitamin hupotea, na hivyo kutokua na faida yoyote. Lakini pia upatikanaji wa hivyo vyakula ni changamoto kwa baadhi ya watu kutokana na mazingira wanayoishi au majukumu ya kazi wanazo zifanya hujikuta wakitumia vyakula ambavyo vipo kwenye supermarkets ambavyo vimesindikwa na kemikali ili visiharibike. Lakini kama utaweza kuhimiri changamoto hii, itakua ni rahisi kwako kutekeleza diet hii kama inavyotakiwa.

MPANGILIO WA MLO WAKO

Mlo wako inatakiwa uendane na mfumo wako wa maisha. Kuna wale ambao shuguli zao za kila siku zinatumia nguvu nyingi au akili nyingi wakati wa asubuhi hadi mchana, na kwa sehemu kubwa watu wengi mfumo wao wa maisha upo hivi; asubuhi hadi mchana ndipo muda mwingi hutumika katika shughuli mbalimbali ambazo zinahitaji nguvu na akili nyingi, na kwa maana hiyo hata sehemu kubwa ya kaloli hutumika muda huu ukilinganisha na jioni na usiku. Hivyo basi hakikisha asubuhi unapata mlo wako wa kifungua kinywa ipasavyo, usiache kupata kifungua kinywa, una weza kupata chakula cha kutosha hali kadhalika mchana wakati usiku ukipata chakula kidogo ukilinganisha na mchana na asubuhi.

AINA YA VYAKULA

Kimsingi kama unataka kupata matokeo mazuri katika kupungua uzito, hakikisha unapunguza kiasi cha vya kula vya wanga na mafuta, huku ukiongeza vyakula vyenye protini. Vyakula vya wanga huongeza uzito kwa kasi zaidi ukilinganisha na vyakula vya mafuta na protini. Hivyo ni vema kuhakikisha katika mlo wako unapunguza wanga. Lakini pia kumbuka kuzingatia nilichokisema hapo juu kwamba wakati wa usiku inatakiwa usipate chakula kingi ukilinganisha na mchana na asubuhi. Hivyo basi angalia ni vema chakula cha usiku kikawa na protini pekee au na mafuta kidogo, lakini chakula cha mchana kiwe na wanga kiasi na mafuta pia, kwasababu wakati wa asubuhi na mchana ndipo ambapo utatumia sehemu kubwa ya chakula ulichokula.

Kwahiyo kitu cha msingi ni kuhakikisha unaweza kuvipata vyakula hivyo; vyakula vya wanga ni kama mahindi, mtama, mihogo, viazi, ngano, mikate, mtama, mchele, keki, ndizi, nyama, mikate, vitumbua, n.k.

Mfano wa vyakula vya mafuta ni kama parachichi, karanga, korosho, mbegu za alizeti na siagi. Lakini pia kuna nyama nyekundu ambazo zina kiasi kikubwa pia cha mafuta.

Vyakula vyenye protini ni kama vile nyama, makundekunde kama soya, kunde na maharage; pia kuna samaki, senene, mayai, maziwa na vyakula vinavyotokana na maziwa kama jibini na maziwa mgando

ASUBUHI

Ukiamka, pata glass ya maji ya kawaida tu. Kisha nenda kafanye zoezi kwa walau dakika 30.  Fanya mazoezi yanayohusisha mwili mzima kutumika, kama vile kuruka kamba kwa dakika 15 au kukimbia. Kisha fanya push ups walau 10 hadi 20, kisha malizia kwa kunyanyua vitu vizito. Sio lazima uende gym, hapana. Unaweza kununua dumbbells ambazo zina uzito unaoendana na wewe. Dumbbells hizi huuzwa kwa bei tofauti kulingana na uzito wake.  Mazoezi ya kunyanyua vitu vizito husaidia kuweka misuli vizuri, ili hata ukipungua uzito usiwe na manyama uzembe.

Baada ya hapo nenda kapate kigungua kinywa (breakfast) ambayo itakuwa na mchanganyiko wa wanga, protini na mafuta. Usisahau kua na matunda kadhaa au saladi katika breakfast yako. Hakikisha una protein ya kutosha kuliko wanga. Kwa lugha rahisi namaanisha hutakiwi kula chapatti au maandazi au vitumbua vingi.

Inashauriwa breakfast yako uipate asubuhi sio zaidi ya saa nne. Ukichelewa kupata breakfast kuna uwezekano mkubwa ukavuruga ratiba yako ya kula chakula cha mchana na usiku.

MCHANA

Chakula cha mchana hutakiwi kupata huu mlo zaidi saa kumi. Hakikisha unapata kuanzia saa saba hadi saa kumi. Mlo huu uwe wa kutosha lakini unaweza kuzidiwa kidogo na breakfast. Kwasababu sehemu kubwa ya chakula utakacho kula mchana, hakitatumika, siku inakua inakaribia kuisha. Hivyo chakula kitahifadhiwa mwilini na baadae kukufanya uongezeke uzito. Kwahiyo ni muhimu kuhakikisha unapata chakula cha wastani. Lakini pia zingatia kupata chakula chenye protein ya kutosha na vitamins na madini ya kutosha kutoka kwenye mbogamboga na matunda.

JIONI/USIKU

Kama utaweza, jioni jitahidi pia kufanya mazoezi. Inaweza kua ni kukimbia, kuogelea, kuruka kamba, weight lifting n.k. Haya ya takusaidia kuchoma mafuta au kaloli ulizoziingiza kupitia chakula cha mchana. Lakini pia itakusaidia kuuweka mwili sawa na kupata hamu ya kupata chakula cha usiku vizuri.

 

Chakula cha usiku kiwe chepesi, inaweza kua ni mchemsho, na mboga za majani na matunda au unaweza kula wali au ugali lakini kwa kiasi kidogo sana. Lakini pia kumbuka chakula cha usiku ndiyo kinatakiwa kiwe cha uwiano mdogo sana ukilinganisha na chakula cha mchana na asubuhi.

Mpangilio huu utakusaidia kupungua uzito taratibu.

ZINGATIA

Miili yetu inaingiza sumu na takataka nyingi sana mwilini kuputia njia mbalimbali, mfano ni kupitia vyakula tunavyokula, maji, hewa na kadhalika. Kwa wastani binadamu huingiza takribani lita mbili za sumu mwilini kwa mwaka. Hizi sumu na takataka sio Salama kabisa kwa afya zetu. Lakini pia huchangia kwa kiasi kikubwa sana kuongezeka uzito. Kwasababu Mwili ukiwa mchafu hupelekea mafuta kuzalishwa kwa wingi mwilini uli kutoa ulinzi kwa Mwili  dhidi ya sumu hizo. Na hivyo kujikuta umeongezeka uzito. Na pia sumu hizi hupelekea mwili kuwa na tabia ya kupenda au kuvutiwa na vyakula au vinywaji vyenye sumu nyingi kama vile soda, keki, chips n.k vyakula na Vinywaji ambavyo vinaongeza uzito kwa kasi sana.
Hivyo basi ni muhimu kufanya Body Cleansing kabla ya kuanza Safari yako ya kudhibiti uzito.

Kwa maelezo zaidi piga simu au nitumie msg whatsapp (+2557160141) au bonyeza kitufe cha "GET IN TOUCH"

Yours truly,

Lusajo

SABABU TANO ZA KUTUMIA “DIET PLAN” HII NA MAZOEZI HAYA KUPUNGUA UZITO

 

 

 SABABU TANO ZA KUTUMIA “DIET PLAN” HII NA MAZOEZI HAYA

Ni dhahiri kwamba tatizo au changamoto au magonjwa yatokanayo na uzito uliopitiliza ni mkubwa sana. Shirika la afya duniani (WHO) linaripoti kuwa hadi kufikia mwaka 2016, asilimia 39 ya wanawake na asilimia 40 ya wanaume walikua na uzito uliopitiliza. Na pia inaripotiwa kuwa  idadi ya watu wenye tatizo la uzito uliopitiliza umeongezeka kwa zaidi ya mara tatu kutokea mwaka 1975 hadi 2016. Hakika, Uzito ni Changamoto kubwa inayotishia usalama wa afya za watu duniani.

Sasa linapokuja suala la namna gani watu waweze kupunguza uzito, wengu huzani ni kitendo ambacho kinafanya mara moja au mara mbili katika maisha yao. La hasha, kupungua au kudhibiti uzito ni kitendo cha maisha yako yote. Kila siku inatakiwa uwe msimamizi mzuri wa namna gani unaweza kudhibiti uzito wako uongezeke au namna gani uweze kupunguza uzito wako; kwasababu madhara ya uzito mkubwa ni  mengi mno na hulewa matatizo ambayo ni ya kudumu na hivyo kuathiri ubora wa maisha yako.

Hivyo basi, kwakua kupungua au kudhibiti uzito ni kitendo cha maisha yako yote, ni muhimu kuangalia njia ambazo ni rahisi kufit mfumo wako wa maisha ya kila siku lakini pia ambazo ni salama kwa afya yako. Huwezi ukawa unashindia mkate na chai ya rangi au maji ya ndimu kila siku. Ni lazima utachoka tu na pia utapata madhara ya kiafya.

Makala hii imekuandalia suruhisho la changamoto hii, kwasababu nitakupatia diet plan na aina ya mazoezi ambayo yatakusaidia sio tu kupunguza uzito wako bali pia kudhibiti uzito wako usiongezeke. Diet plan hii ni ALOE VERA DIET PLAN maarufu kama FOREVER C9 na F15.

Forever C9 na F15 ni mpangilio wa ulaji na ufanyaji mazoezi utakao kusaidisa katika safari yako ya kudhibiti uzito. Ina mchanganyiko wa virutunbisho vingi na tofauti tofauti

Sababu tano kwanini utumie diet plan ya forever c9

1. Inasaidia sana kuondoa sumu na kuimarisha afya ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula Mmeng’enyo wa chakula ni miongoni mwa mifumo michafu sana.

Na imekua ikichangia kwa kiasi kikubwa kuleta magonjwa kwa wanajamii. Forever C9 na F15 zina kinywaji kinaitwa Forever aloe vera gel. Kinywaji hiki kinauwezo mkubwa wa kusafisha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ili kuruhusu chakula kumeng'enywa kwa wakati hivyo kuuzesha mwili kupunguza uwezo wa kubadili wanga kuwa mafuta. Husafisha sumu na uchafu utokanao na vyakula, vinywaji, hewa, dawa za hospitali mfn.chips, vumbi, AC, hivyo kuupa mwili nafasi ya kuunguza mafuta. Pia kuimarisha kinga ya mwili kwani hulisha seli moja kwa moja. Hiki kinywaji kitakupa msingi mzuri wa kuanza safari yako ya kudhibiti. Mwili ukiwa safi ni rahisi sana kupungua uzito.

2.  Inasaidia kuupa mwili joto na hivyo kuweza kuchoma mafuta mwilini.

Joto la mwili ni muhimu sana katika kuwezesha kuyeyusha mafuta mwilini. Na hivyo basi ni rahisi mtu kuweza kupunguza sehemu za mwili ambazo mafuta yamehifadhiwa kwa wingi. Inaweza kua kitambi au mapaja n.k. Diet plan ya Forever C9 na  F15 ina kirutubisho kinaitwa Forever Therm ambacho kazi yake kuu ni kuupa mwili joto hasa unapofanya mazoezi. Na hivyo hua rahisi kupunguza uzito.

3. Inasaidia kuweka sawa hamu yako ya kula.

Kwa watu wengi ambao wana uzito mkubwa hua wanakua na hamu ya kula iliyopita kiasi, hivyo basi hua ngumu kwao kukaa bila kula. Kwahiyo diet plan hii itakusaidia kuweza kuidhibiti hamu yako ya kula hovyo kwasababu ina kirutubisho kinachoitwa Forever Garcinia plus.Hubadili mafuta yaliyotunzwa mwilini kuwa nishati hivyo kuruhusu mwili kutumia akiba ya chakula kilichopo na kupunguza hitaji la chakula toka nje. Pia hupunguza hamu ya kula ovyo kwani hutoa taarfa kupitia nerves juu ya kutosheka kwa mwili hivyo hurahisisha upunguaji.

4. Inasaidia kuimarisha uwezo w ufyonzwaji wa virutubisho

 

Watu wengi wanachangamoto za kutopata choo, kupata choo kigumu, tumbo kujaa gas. Watu wenye matatizo haya hua ni ngumu kupungua uzito. Hivyo basi ni vema kuhakikisha changamoto za kutopata choo zinatatulika, na hapo itakua rahisi kupungua uzito au kuudhibiti.Forever C9 na F15 ina kirutubisho kinaitwa Forever fiber. Kirutubisho hiki ni nyuzi nyuzi mhimu kwaajili ya kuboresha mfumo wa usagaji chakula kwani husaidia bacteria rafiki ktk utumbo kuzaliwa hivyo kuufanya utumbo kumeng'enya chakula kwa urahisi. Pia Hukaa tumboni kwa mda mrefu hivyo kukufanya ujihisi kushiba na hatimae kuepuka kula vyakula mara kwa mara.

5. Inasaidia kuupa mwili protein ya kutosha na hivyo kukupa afya njema na kukupa mng’ao mzuri.

Lakini pia hukaa tumboni kwa muda, na hivo kukusaidia usipende kula kula tu. Diet plan yetu ina powder shake iliyotokana na soya ambayo ni protein nzuri sana. Huu ni mchanganyiko wa unga wenye protein ya mimea kama soya beans, husaidia kuimarisha misuli na kuboresha seli. Ni lishe tosha kwani huujenga mwili kwa nyama baada ya kuondoa mafuta.

Hizi ndiyo sababu tano za kwanini utumie diet plan hii.  Moja ya diets bora kabisa duniani kwa sasa. Itakusaidia kukupa mfumo bora wa maisha ambao utakufanya usiongezeke uzito kirahisi.

 

Forever C9 ni program ya siku tisa iliyoandaliwa maalum kuuandaa mwili wako katika safari ya kupungua uzito, program hii ina bidhaa tano yaani

-Aloe vera gel 2

-Ultra lite vanilla(maziwa) 1

-Forever garcinia

-Forever therm 

-Forever fiber pakiti 9

-tape 1 na kitabu cha mwongozo 1

Kwa maelezo zaidi na namna ya kufahamu mazoezi ambayo utayafanya ili udhibiti uzito wako, nitafute kwa namba +255716160141 (Piga au njoo whatsapp) au bofya button iliyoandikwa "GET IN TOUCH"

Yours Truly,

Lusajo

KWANINI HUPUNGUI UZITO JAPOKUA UNAFANYA SANA MAZOEZI?

Siku zote unapojaribu kupunguza uzito wako mwili nao hupambana kuurudisha katika hali yake ya awali. Kwahiyo unaweza kupungua uzito haraka siku za mwanzo lakini mbeleni kadri unavyoendelea utaanza kupata shida kupungua, utakua unapungua kidogo sana.
Sasa fuatilia kwa makini ni sababu zipi zinaweza kukufanya usipungue uzito kama unavyotarajia au usipungue kabisa.

Continue Reading
 • 1
 • 2

© 2020 The Superteam

Press enter to search
Press enter to search

The Super Team

We support you to Build a successful full-time or part-Time business that fits your schedule and lifestyle, so that you can achieve what matters to you.

(+255) 716 160 141
info@thesuperteam.co.tz
Uhindini Street, Dodoma City Center, Tanzania

Opening Hours

Mon - Fri
9:00 am to 18:00 pm
Saturday
9:00 am to 16:00 pm
Sunday
9:00 am to 16:00 pm

CEO's Words

CEO

We help people just like you build successful businesses. The part-time of full-time business that fits your schedule and lifestyle, so that you can achieve what matters to you.

Get Connected